China and the 2008 Olympic Games : Swahili
CHINA NA MICHEZO YA OLYMPIKI 2008
Barua ya wazi kwa wanaharakati na mawakili wa Darfur
Eric Reeves
February 10, 2007
Kampeni ya hali ya juu iliyoandaliwa kudhihirisha njama na ushiriki wa nchi ya China katika mauaji ya kimbari huko Darfur Sudan iko karibu kuzinduliwa. Hata hivyo huu ni wakati muafaka wa kuanza kufikiria jinsi ya kushirikisha nguvu ya mawazo na ubunifu wa wanafunzi na mawakili wa Darfur katika suala hili muhimu.
Huu sio muda wa maneno ya ubabaishaji na kuandika barua kwa wale walioridhika na kukwepa jukumu la msingi la wakati huu: ambalo ni kubadilisha nguvu ya kidiplomasia ya kimataifa kwa namna ambayo italeta upatikanaji wa amani katika jimbo la Darfur, mkakati utakaoleta usalama wa raia na watoa misaada ya kibinadamu. Bila uhakika wa usalama, mashirika ya misaada ya kibinadamu yataendelea kuondoka na maisha ya maelfu ya watu wa Darfur yataendelea kupotea.
Huu sasa ndio wakati wa kuanza kuikemea China…kudai na kusisitiza kuwa kama Serikali ya Beijing itaandaa tukio hili la hali ya juu na la kimataifa kipindi cha joto mwaka 2008, lazima China iwe ni taifa la watu wanaojali wajibu wao wa kimataifa. Kaulimbiu ya China katika mashindano haya ni “DUNIA MOJA, NJOZI MOJA” Hii haifurahishi na ni kinyume kabisa ukichukulia ushiriki wa Beijing katika njama ya mauaji ya kimbari ya Darfur.(angalia tovuti http://www.olympic.org/uk/games/beijing/index_uk.asp)
Uongozi wa China lazima uelewe kwamba, kama wanakataa kutumia ushawishi wao usio na mpinzani wa kisiasa, kiuchumi na kidiplomasia kwa Serikali ya Khartoum kuhakikisha kuwepo kwa Jeshi lililoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa chini ya kifungu 1706, basi, bila huruma, watapambana na kampeni ya nguvu kuikemea kutokana na ukaidi wake huo.
Ili kufanikiwa, kampeni hii lazima iwe ni ya kimataifa. Hatua muhimu ya kwanza ninaamini kuwa ni kuanzisha ubunifu wa kutafsiri hoja muhimu na tafsiri pana katika lugha mbalimbali na kuzisambaza katika nchi nyingi kama inavyowezekana. Iwapo watu wataelewa uhusiano wa China kama mwenyeji wa mashindano ya michezo ya Olimpiki na China kama mshirika wa siri katika mauaji ya kimbari huko Darfur, wataweza pia kuweka pingamizi katika majukumu haya mawili ya kuvunja moyo. Lakini ni lazima watu waelewe vizuri uhusiano huu.
Tufanyeje? Ufahamu au elimu huleta uwezo na uwajibikaji; Jukumu la msingi ni kuwaelimisha wale ambao kwa hivi sasa hawajui vizuri ushiriki wa China huko Sudan kwa ujumla na hususan Darfur. Baadhi ya mambo muhimu yameainishwa hapa chini. Zaidi ya hayo kuna uchambuzi wa ziara ya kibiashara ya Rais Hu wa China huko Khartoum pamoja na makala mbili za maoni kuhusu “Olyimpiki ya Mauaji ya Kimbari”
Ni muhimu kukumbuka kwamba katika maoni yangu, hii haipaswi kuwa kampeni ya kususia mashindano ya michezo ya Olimpiki. Kususia michezo hii kutaathiri lengo zima la kampeni hii na kuleta mgawanyiko mkubwa. Isitoshe, kama mashindano yatasusiwa (ambayo haitawezekana) jukwaa la kisiasa la kuisuta au kuikemea China litajitokeza. Zaidi ya hapo, kususia michezo ya olimpiki pekee haisaidii kitu: Changamoto lililopo ni kuikemea China kuwawajibisha Viongozi wake, kuwafanya waelewe kuwa kama hawataibana Sudan, harakati hizi zitaongeza nguvu mpaka siku ya Sherehe za ufunguzi.
Walengwa sio wanariadha (wanamichezo). Hakika wanaweza kuhimizwa kuvaa utepe wa kijani wa ukubwa wanaotaka katika mavazi yao kama ishara ya kuunga kwao mkono watu wa Darfur. Hakika wanapaswa kuhimizwa kuongea wazi wazi kwa umma kuhusu Darfur. Lakini wanariadha wa Olimpiki sio walengwa bali utawala wa Beijing. Ni utawala wa China pekee wenye uwezo wa kubadili mtizamo uliopo wa kidiplomasia katika hali ambayo itailazimisha Khartoum kuruhusu kuwepo kwa Jeshi litakalotoa ulinzi kwa waathirika wa mauaji ya kimbari yanayoendelea. China ndiyo mlengwa na wala sio michezo ya olimpiki au washiriki wake.
Nini majukumu ya awali?
Hapa kuna uwanja mpana wa ushawishi-bunifu, na matumizi ya ujuzi mbalimbali na uwezo: Ujuzi wa lugha, matumizi ya internet, michoro, ushawishi, maandishi na mipangilio mingine. Nini kitatokea, kwa mfano, kama wanafunzi 1,000 na mawakili wanaandamana mbele ya ubalozi wa China katika jiji la Washington, DC, wakiwa na mabango na T-shati kwamba China itawajibika kwa njama za ushiriki wake katika mauaji ya kimbari ya Darfur. Nini kitatokea kama maandamano hayo yataendelea, na kuwa makubwa, na kuendelea katika Nchi nyingine nyingi? Nini kitatokea kama kila mahali, popote pale, Mabalozi wa China na Wanasiasa watakutana na wale wanaoshinikiza tukio hili (Mashindano ya Michezo ya Olimpiki) kwa kuweka bayana ushiriki wa China katika mauaji ya kimbari huko Darfur.
Waandishi wa makala wanaopenda au wenye ujuzi wanaweza kutumia picha na video zinazopatikana kirahisi kutengeneza filamu zitakazoonyesha utamaduni wa michezo ya Olimpiki, mauaji ya kimbari ya Darfur na ushiriki wa China katika mauaji hayo. Haitakuwa vibaya kuingiza kiambatanisho cha michezo ya Olimpiki ya mwaka 1936 iliyofanyika Ujerumani chini ya utawala wa ki-Nazi kama mfano wa kielelezo kilichopita cha kulinganisha na suala hili la mauaji ya kimbari ya Darfur. Nafasi ya wanasanaa wa vielelezo, matumizi ya picha na zana nyingine ni pana. Kila kitu kuanzia mafaili ya hali ya juu ya PDF mpaka Screensavers, sticker za magari, mabango, T-shirts na vikombe vya kunywea kahawa vinaweza kufikisha ujumbe.
Kufanya tafsiri ni jukumu la msingi: Hii siyo kampeni ya Amerika au nchi za Magharibi. China lazima iguswe kwa kukemewa kutoka kila upande. Watu walio na uwezo mkubwa wa lugha –Kifaransa, Kispanish, Kiarabu, Kichina, Kijapani, Kikorea, Kiswahili, Kijerumani, Kitaliano, Kirusi, Kihangari, Kichek, na lugha nyingine—wanapaswa kuanza kutumia ujuzi wao kutafsiri maandiko ya msingi na ushawishi kutoka katika lugha ya Kiingereza. Wale walio na mahusiano na watu katika nchi nyingine wanapaswa kuanza mawasiliano ili kuanzisha ushawishi katika njanja za kimataifa kama inavyowezekana. Kitengo cha haki za binadamu katika China (http://www.hrichina.org/public/index) kinaweza kuwa ndicho chenye uwezo zaidi wa kuingiza suala hili nchini China. Kuna njia nyingine pia za kungiza kampeni hii nchini China.
Kuandika barua na kampeni za rufaa ambazo zitaiamsha kamati ya kimataifa ya Olimpiki (http://www.olympic.org/uk/index.uk.asp) kwa matendo haya mawili yanayoiaibisha China yaani kuendeleza Mauaji ya kimbari Darfur na wakati huo huo kuwa mwenyeji wa Michezo ya olyimpiki. Hii pia itaanzisha kampeni sawa na hii kwa kushinikiza wafadhili wa Shirika la Olyimpiki kutumia uwezo wao kutafuta muafaka na China. Ni muhimu hivi sasa kukamilisha makubaliano na wafadhili wa Shirika la Olympiki.
Ili kufanikiwa, kampeni hii lazima isambae kama “virusi”. Lazima iwe na nguvu, iwe na ubunifu, ilenge na isiingiliwe. Kampeni hii lazima itumie faida zilizopo sasa hivi za technologia ya mawasiliano. (nitatoa mawasiliano kupitia website yangu, www.sudanreeves.org kwa ajili ya matumizi mazuri yenye ubunifu). Wachina lazima walazimishwe kuona kuwa kuna uchaguzi mgumu mbele yao: Ni juu yao kuamua kuishinikiza Sudan kuruhusu jeshi la kulinda amani kama ilivyoamuliwa na Umoja wa Mataifa azimio la 1706 au ikumbane na kampeni ya kimataifa yenye nguvu kuliko zote katika historia ya kimataifa ya kuikemea. Wachina lazima waelewe kuwa hakuna njia mbadala. Hakuna njia ya tatu.
Ukosefu wa ushawishi wa jumla wenye matokeo haujapotea katika mauaji ya kimbari yasiyo na huruma Khartoum. Pamoja na umaarufu na nguvu ya Wanaharakati wa Marekani-Darfur na nguvu kubwa ya kampeni yenye mafanikio inayoongozwa na Marekani, ni lazima msukumo ulenge ngazi za juu. Makampuni mengine ya Ulaya ni vyema yakafuata mfano wa kampuni ya Siemens ya Ujerumani, ABB Ltd ya Uswisi, kampuni ambazo hivi karibuni zimesimamisha kazi zake huko Sudani kama Jumuiya ya kimataifa ilivyoagiza. Haya ni mafanikio makubwa kitaifa. Kuendelea kupata hasara ya kibiashara na uwekezaji wa namna hii, kwa uhakika unawafurahisha viongozi wa National Islamic Front. Lakini hasara za namna hii lazima zijumuishwe na shinikizo za kidiplomasia kutoka China ambayo ndiyo mshirika mkuu wa kiuchuni na muwezeshaji wa Kijeshi na hivyo kuiweka kinga ya kidiplomasia. Jukumu hili ni la kukatisha tamaa lakini linawezekana iwapo kuna utu wa upendo na ubunifu wenye nguvu katika Jamii ya Ushawishi ya Darfur.
Natuanze kampeni hizi!
***************************

















